Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:38 pm

NEWS: BAVICHA WATANGAZA MAANDAMANO

KAGERA: BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Mkoa wa Kagera limetangaza kuandaa maandamano ya amani kulaani tukio la kushambuliwa kwa risasi Mwanasheria Mkuu wa chama chao, Tundu Lissu Septemba 7, mwaka huu.


Mwenyekiti wa Bavicha Manispaa ya Bukoba, Ishengoma Audax alisema licha ya kuandamana watakwenda katika Hospitali ya Rufaa Bukoba kuchangia damu.


Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kagera, Francis Rutta alisema wameamua kuandamana kulaani kushambuliwa kwa Lissu na kuvitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinawakamata na kuwatia mbaroni wahusika.


“Tunafanya maandamano ya amani hivyo hatutegemei polisi kuzuia maandamano yetu kwa kuwa ni ya amani.


“Lakini tunaunga mkono uamuzi wa Brlaza Kuu la Taifa Bavicha linaloongozwa na Mwenyekiti Patrobas Katambi,” alisema.


Alisema wamekuwa wakishangazwa na hatua ya polisi kuwazuia wananchi kumuombea Tundu Lissu ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa makada wa chama chao waliovaa fulana zenye ujumbe wa kumuombea.


Alisema huo ni ukiukaji mkubwa wa demokrasia.