November 26, 2024, 3:43 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BASI LA ABOOD LAPATA AJALI MWANZA
Basi la Kampuni ya Abood Bus Service ambalo linafanya safari zake kati ya Dar es salaam kwenda Mwanza limepata ajali asubuhi ya leo Agosti 9, 2019 katika maeneo ya Mkolani njee kidogo na jijini la Mwanza.
Taarifa kutoka kwa Mashuhuda wanasema chanzo cha ajali hiyo ni mwendesha pikipiki (bodaboda) kuingia barabarani ghafla bila ya tahadhari hivyo kusababisha dereva wa basi kupoteza mwelekeo
"Huyu boda alikatiza ghafla barabarani alikuwa anamuwahi mteja wake, na alivuka bila kuangalia nini kinakuja" amesema Rashidi Iddi (shuhuda )
Katika ajali hiyo taarifa za awali zinasema kuna kifo cha mtu mmoja ambaye ni dereva wa pikipiki huku watu kadhaa wakijeruhiwa.