- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BASHIRU AHIDI KUMNG'OA ZITTO KABWE KIGOMA MJINI
Kigoma. Katibu Mkuu wa chama Cha Mapinduzi CCM, Dk Bashiru Ally amesema wao kama chama wanajipanga kuibuka na ushindi wa ubunge katika jimbo la Kigoma Mjini linaloongozwa na Mbunge ACT Wazalendo Zitto Kabwe.
Dk Bashiru amesema wapo tayari kulirejesha jimbo hilo mikononi mwa CCM kwa gharama zozote katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2020.
Akizungumza leo Jumapili Januari 19, 2020 manispaa ya Kigoma Ujiji katika mkutano na wanachama wa CCM na kugawa vitambulisho kwa mabalozi, Dk Bashiru amesema jimbo hilo kwa muda mrefu limekuwa mikononi mwa wapinzani.
"Sababu tunayo, nia tunayo na malengo tunayo hakuna atakayeweza kuturudisha nyuma kwa kasi yetu tunayoendana nayo," amesema Dk Bashiru.
Jimbo hilo la Kigoma Mjini kuanzia Mwaka 2010 hadi 2015 mbunge wa Kigoma Mjini alikuwa Peter Serukamba wa CCM ambaye katika uchaguzi wa mwaka 2015 alikwenda kugombea jimbo la Kigoma Kaskazini ambalo Zitto ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo akienda kugombea Kigoma Mjini.