- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BASHE AITAKA SEREKALI KUIPOKEA RIPOTI YA IMF ILIYOVUJA
Dodoma. Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe ameitaka serekali kuipokea Ripoti iliyovuja ya Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) kwasababu ripoti hiyo inaonesha ina dira nzuri ya kuisaidia Serekali, ili iweze kujipanga vizuri huko mbeleni.
Bashe amesema ripoti hiyo inamambo mazuri ndani yake.
Kauli ya Bashe ameitoa leo bungeni Jumanne Mei 14, 2019 wakati akichangia hotuba ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka 2019/20.
Pia amezungumzia suala la viwanda akisema kuwa wafanyabiashara wa hapa nchini Tanzania wanapata shida kubwa katika uanzishaji wa viwanda kutokana na utitiri mkubwa wa kodi. Bashe ametolea mfano kwa mtu anayeanzisha kiwanda cha madawa, anapaswa kuwa na leseni 26 sawa na anayeanzisha kiwanda cha maziwa.
Aidha amezungumzia kuporomoka kwa biashara kumekuwa hakuelezeki akitolea mfano wa ngozi ambazo mwaka 2006 zilizosafirishwa zilifikia 1.2 milioni lakini kwa sasa ni 200,000 tu