- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BASATA "HATUWATAMBUI STEVE NYERERE NA IRENE UWOYA"
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limesema wasanii Steve Nyerere na Irene Uwoya hawajasajiliwa na baraza hilo kufanya shughuli za sanaa.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Julai 17, 2019 na kaimu katibu wa baraza hilo, Onesmo Kayanda baada ya kumalizika kwa kikao kati ya baraza hilo na wasanii hao.
"Tumezungumza nao mambo mbalimbali lakini katika maongezi pamoja na mambo mengine tumegundua hawakusajiliwa na baraza na tayari tumewapa maagizo wafanye hivyo mara moja," amesema Kayanda.
Kuhusu Uwoya kuwarushia fedha wanahabari katika tukio lililotokea juzi Jumatatu Julai 15, 2019, Kayanda hakutaka kuweka wazi jambo hilo.
“Tunalaani kitendo hicho kwa nguvu zote na tumekuwa tukifanya hivyo mara zote kuwaasa wasanii kufanya mambo yenye kujenga jamii badala ya kuibomoa, ”amesema.
Kwa upande wake Steve amesema “Nawaomba msamaha waandishi wa habari na Serikali kwa ujumla, kuhusu vifaa vilivyoharibika tumeanza kuzungumza na baadhi yao na tunalifanyia kazi suala hilo.”
Akifafanua kwa nini Basata imewaita wasanii hao wakati si wanachama wao, mwanasheria wa Baraza hilo, Onesmo Ndinga amesema adhabu za wasanii wasiojisajili na kuendelea kufanya shughuli za sanaa zipo nyingi mojawapo ni hiyo ya kuwaita