- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BARUA PEPE ZILIZOVUJA ZAMUWEKA KUTI KAVU RAIS RAMAPHOSA
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesisitiza kuwa hana kosa lolote baada ya kuvuja kwa barua pepe ZAKE kuhusu mchango aliopokea wakati wa kampeni ndani ya chama cha ANC mwaka 2017.
Mwishoni mwa mwezi Julai rais Cyril Ramaphosa alisema ataenda mahakamani kupinga ripoti ya ofisi ya msimamizi wa mali za umma ambayo ilimtaja kudanganya bunge kuhusu kupokea fedha za michango kusaidia kampeni yake mwaka 2017.
Kwenye ripoti hiyo Ramaphosa anadaiwa kupokea kiasi cha randi laki 5 kusaidia kampeni zake kinyume na maadili ya utumishi wa uma.
Tayari mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi wa mali za uma, Busisiwe Mkhwebane ametoa taarifa akiunga mkono hatua iliyochukuliwa na rais Cyril Ramaphosa.
Awali Ramaphosa aliesema baada ya kuisoma kwa kina alibaini kuwa ripoti hiyo ina makosa na tuhuma za kupikwa na kutaka mara moja ifanyiwe mapitio na mahakama za nchi hiyo.