- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BARAZA LA WADAU WA MAZIWA WALAANI UKIMYA WA BODI YAO
DODOMA: WAJUMBE wa baraza la wadau wa maziwa Tanzania wamelalamikia kitendo cha kukaa muda wa miaka mitatu sasa bila kuwa na bodi ya maziwa.
Wajumbe hao walitoa malalamiko yao muda mfupi baada ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi,William Ole Nasha,kufungua mkutano wa 13 wa baraza hilo lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Veta mjini hapa.
Mjadala huo kwa kukosekana kwa wajumbe wa bodi ya maziwa ulizuka baada ya Dk.Aichi Kitilyi ambaye ni mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa kutoa maelezo kuwa hataweza kujibi jambo lolote katika mkutano huo kutokana na kuwa mpaka sasa bodi haina viongozi .
Dk.Aichi amesema tangu kumalizika kwa mkutano wa kumi na mbili uliofanyika Mkoani Manyara haukuwa na viongozi wa bodi licha ya kuwa maombi tayari yameisha tumwa kwa waziri husika.
“Kutokana na kuwa mpaka sasa bodi ya maziwa haina viongozi mimi hapa siwezi kujibu jambo lolote ambalo lilitokana na mkutano wa baraza la wadau wa maziwa ila ninaweza kutoa ushauri kama mdau wa kawaida nah ii ni kwa mujibu wa sheria inayounda bodi ya maziwa” alisema Dk.Aichi.
Naye mwenyekiti wa Muda wa baraza la wadau wa maziwa Jonh Mnyikasi,amesema kuwa kutokana na kutokuwepo kwa uongozi wa bodi kwa muda wa miaka mitatu sasa kuna haja ya mkutano huo kujadili jambo hilo na kulitolea tamko.
“Kimsingi kuna haja ya wajumbe kujadili jambo hili kwa kina zaidi ili kuhakikisha tunatoa tamko juu ya kuwepo kwa viongozi wa bodi, kama hatuwezi kuwa na viongozi wa bodi hatuwezi kuwa na uendelezi mzuri wa utendaji wa kazi.
“Hapa tunaona sasa mwenyekiti wa bodi yupo hapa lakini amekuja kwa sababu ya mapenzi yake na nia njema ya kulipenda baraza la wadau wa maziwa lakini hawezi kujubu jambo lolote linalohusiana na mambo ya bodi ila kama alivyosema anaweza kutoa ushauri kama mdau na siyo kama mwenyekiti wa bodi” alisema Mnyikasa.
Akifungua mkutano wa 13 wa baraza la wadau wa maziwa Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi ,William Ole Nasha alisema kuwa licha ya kuwa Tanzania kuwa na mifugo mingi lakini bado hakuna uzalishaji wa maziwa wenye tija.
Alisema bado kuna changamoto mbalimbali zinazogusa sekta ya maziwa ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mazingira mazuri ya uzalishaji na usindikaji wa maziwa katika hali mbalimbali sambamba na kukosekana kwa vifungashio salama .
Ole Nasha amesema kuwa tasnia ya maziwa kwa sasa inazalisha asilimia 2.5 kwa pato la taifa,na zao la maziwa ni zao ambalo linaweza kutoa pato zuri kwa mtu binafsi,kaya na taifa kwa ujumla .
Mbali na hilo Ole-Nasha amesema kuwa licha ya kuwa Tanzania ni nchi ya pili Afrika kuwa na mifugo mingi lakini bado kuna uhaba mkubwa wa ng’ombe wa maziwa ambapo kwa sasa ng’ombe wa maziwa kwa sasa ni laki 7.8 tu .
“Wadau wa maziwa mnatakiwa kutambua kuwa maziwa yanaweza kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja,kaya pamoja na taifa kwa ujumla hivyo kama maziwa yataweza kupewa kipaumbele, huku wakijitahidi kuondokana na changamoto mbalimbali ambazo wanakumbana nazo” alisema Ole-Nasha.