Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:34 am

NEWS: BARAZA LA MAASKOFU CONGO LIMEENDELEA NA MSIMAMO WAKE WA UCHAGUZI

Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Cenco), limesema limekubaliana na matokeo ya urais , lakini hata hivo limesisitiza kuwa ukweli wa matokeo yenyewe umekataliwa.

media

Maaskofu wametoa wito kwa viongozi wapya nchini DRCongo kufanyakazi kwa bidii kurejesha utawala wa kisheria.

Cenco imeendelea kusisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi wa rais kama ilivyochapishwa na Tume huru ya taifa ya Uchaguzi (CENI), hayafanani na takwimu zilizokusanywa na ujumbe wake wa uchunguzi.

Baraza hilo la maaskofu limetangaza kwamba litaendelea na uchunguzi wake wa uchaguzi na mpango wa elimu ya kiraia kama anavyoeleza hapa Dontien Nshole Katibu mkuu wa baraza la maaskofu Cenco.

Hata hivyo upande wa utawala mpya, umesema muda huu sio wa mjadala kuhusu uchaguzi, bali ni muda wa kufanya kazi.