- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BARAZA LA HABARI WAITAKA POLISI KUTENDA HAKI MWANDISHI KABENDERA
Baraza la Habari Tanzania(MCT), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania(UTPC), Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa pamoja wametoa tamko kuhimiza uzingatiaji wa haki stahiki kwa watuhumiwa Hasa kwa mwandishi wa habari za kiuchungizi Bw. Erick Kabendera
Jumuia hizo zimewaomba maofisa wa uhamiaji wamrudishie Bwana Erick Kabendera, Mke na Watoto wake hati zao za kusafiria ikiwa hawakuthibitisha kuwa Bwana Erick si raia wa Tanzania;
"Tunalisihi Jeshi la Polisi kufuata utaratibu katika kukamata watu , ikiwemo kuwataarifu sababu za kukamatwa, ndugu wafahamu kituo cha polisi alichopelekwa na kushikiliwa ili kuepuka sintofahamu na kudhaniwa kuwa mtu ametekwa kumbe amekamatwa na vyombo vya usalama;"
"Maofisa wa jeshi la Polisi watoe haki zote za mshatakiwa kama kuonana na mwanasheria pamoja na familia yake pindi wanapokua wanawashikilia watuhumiwa;
Maofisa wa Jeshi la Polisi wajiepushe na vitendo vinavyoweza kuashiria ukiukwaji wa haki za watuhumiwa kama uteswaji au udhalilishaji wa namna yoyote;
Polisi wahakikishe wanawapeleka washtakiwa mahakamani ndani ya muda uliowekwa kisheria;"
" Umemkamata mtu unamtuhumu kwa kosa hili kuna sababu gani ya kutaka asijulikane yupo wapi, " Katibu Mtendaji MCT, Kajubi Mukajanga.
Wito kwa wanasheria wote nchini kutafakari na kuchukua hatua ya kupinga sheria ya utakatishwaji fedha na uhujumu uchumi haswa katika suala la dhamana;
Katika kipindi hiki ambacho serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria, inapitia upya Mfumo wa Haki Jinai nchini, wanasheria na Watetezi wa Haki za Binadamu kote nchini wanapaswa kupinga nguvu na mamlaka makubwa aliyopewa mwendesha mashtaka wa serikali (DPP) katika kuendesha kesi hizi na haswa katika upatikanaji wa vielelezo na ushahidi mbalimbali katika mashtaka ya aina hii;
Makosa yote yawe na dhamana. Sheria zote zinazominya haki ya watuhumiwa kupata dhamana zifanyiwe marekebisho ili kuwapa watuhumiwa haki yao ya kuwa huru wakati vyombo vya usalama vinapoendelea na uchunguzi au Mahakama inapoendelea na kesi.
Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lipitishe sheria itakayoruhusu makosa yote yawe na dhamana.
Mahakama ipewe mamlaka ya kutoa maamuzi kuhusu dhamana. Sheria zisizuie dhamana bali mahakama iamue kuhusu dhamana ya mtu kulingana na mazingira na uzito wa shauri.
Masharti ya dhamana katika mahakama zetu na Jeshi la polisi yalegezwe ili kuweka masharti nafuu yatakayowawezesha watuhumiwa kupata haki yao ya dhamana.
Jeshi la Polisi na vyombo vyote vinavyohusika na utoaji haki visikamate watuhumiwa kabla ya kumaliza upelelezi. Tunaungana na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma ya kuhakisha watu hawakamatwi hadi pale uchunguzi wa kutosha uwe umefanyika. Hii itapunguza muda mwingi wa watuhumiwa kukaa mahabusu.
Sheria itamke wazi kwamba ikifika kipindi fulani cha muda na upelelezi haujakamilika basi kesi ifutwe.
Tunapendekeza kuwepo utaratibu wa polisi kupeleka shauri la kusikiliza ushahidi (evidential Hearing). Hii itasaidia upatikanaji wa haki na kwa wakati. Katika mchakato huu polisi wanatakiwa kuleta shauri hilo wakiwa na vielelezo vyote na ushahidi wote mbele ya mahakama. Mahakama isikilize na mtuhumiwa ajibu ndipo mahakama ikiridhishwa kuwa mtuhumiwa ana kesi na anaweza kutiwa hatiani itoe amri ya kukamatwa mtuhumiwa. Shauri hili litasaidia kupunguza muda ambao polisi wanatumia kufanya upelelezi huku mtuhumiwa akinyimwa haki zake za msingi ikiwa kudhaniwa hana hatia mpaka atakapokutwa na hatia, vilevile ushahidi ukiwa umekamilika kesi itaendelea kwa haraka na haki itapatikana.