- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BARAZA LA CHADEMA WATANGAZA VITA NA SERIKALI YA CCM
DODOMA: BARAZA kuu la Chama Cha Demokrasia Maendeleo (Chadema)limetangaza msimamo wake wa kutokuendelea kunyamaza na kulalamika dhidi ya vitendo vya kidikteta na unayanyasaji wanaofanyiwa na serikali iliyopo nadarakani.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe wakati wa ufunguzi wa baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa African Dream mjini hapa.
Mbowe amesema kuwa Chadema ni vyama kati ya vyama ambavyo vinapenda amani na kuenzi utulivu wa anchi na chama hicho hakipo tayari kuona watanzania wanafarakana na kumwaga damu lakini kutokana na vitendo vya kidhalimu vinavyofanywa na Serikali ya CCM sasa wanaazimia kuwa na msimamo wa kupinga na kukataa unyanyasaji unaofanywa na watawala madikteta.
Katika mkutano huo wa Baraza wa kikatiba ambao ufanyika mara moja kwa mwaka wajumbe 332 waliudhuria kati ya wajumbe 370 ya wajumbe wote sawa na asilimia 89.7.
Mbowe amesema kwa sasa nchi haiko salama kutokana na matamko mbalimbali ambayo yanafanywa na kiongozi wanchi huku akiwa shujaa katika kukanyaga katiba na kuzima demokrasia kwa kuzuia shughuli za siasa hasa upinzani kufanya kazi zao.
“Viongozi wenzangu nataka mjue kabisa kuwa tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama kwa kipindi cha miaka 25 sasa lakini yapo mambo mengi ambayo viongozi wamekutana nayo,wapo wengine ambao wamepoteza maisha,wapo waliokuwa walemavu na wapo waliopoteza mali zao.
“Tumeendelea kupambana hadi sasa hapa tulipo, lakini ndugu zangu sasa mnaona utawala wa sasa wa awamu ya tano unavyofanya kazi kwa maonevu makubwa,kwa kukanyaga katiba ya nchi kuvunja sheria ya nchi ikiwa ni pamoja na kukandaniza na kuminya demokrasia.
“Kutokana na hali hiyo sasa baraza tunatoka na azimio moja ni bora sasa mmoja aondoke lakini tuhakikishe tunajenga heshima ya demokrasia ambayo inaonekana kukanyagwa na kuminywa na mtawala aliyepo madarakani kwa sasa.
“Tumekuwa na rais ambaye anavunja katiba ya nchi anaendesha nchi kwa jinsi anavyotaka na kibaya zaidi amekuwa mtu wa kuwaonea watanzania kwa kutoa matamko ambayo yahaendani na demokrasia watu wanauliwa bire kila kukicha utekaji sasa nasema hatuwezi kuendelea kulalamika na haki haiombwi bali inadaiwa na inatafutwa sasa bora mmoja aondoke ili demokrasia iendelee” alisema Mbowe huku akishangiliwa na wajumbe.
Hali ya kisiasa.
Katika baraza hilo Mbowe amesema hali ya kisiasa hapa nchini siyo nzuri kwani imegubikwa na hali ya sitofahamu kutokana na tuwala wa kimabavu na usiofuata misingi ya utawala bora.
Amesema kwa sasa nchi haiko salama kwani kama nchi inakuwa na kiongozi ambaye anaongoza nchi kwa ubabe hasikilizi watu ni wazi kuwa kinachofanyika ni kutotimiza utawala wa kisheria ikiwa ni pamoja kuendesha nchi kwa mabavu na unyanyasaji wa hali ya juu zaidi.
Amesema ili kuthibitisha kuwa usala wa kisiasa ni ndogo nchini ni kutokana na watu kutekwa na kupotezwa katika mazingira magumu ambayo kimsingi ni mazingira tata .
“Naomba mkumbuke yupo wapi Beni Saanane, nimejionea kuwekwa ndani na kunyimwa dhamana mbunge wa Arusha Godbles Lema, Meya wa Jiji la Arusha, Kufunguliwa mashitaka Lijuali kali pamoja na viongozi mbalimbali kutokana na visa tu pamoja na chuki ya mtawala mmoja ambaye anafanya kazi kwa matakwa yake mwenyewe.
“Iwe kwa kujua au kutokujua au washauri wake kutomshauri sasa hali ya kisiasa imekuwa mbaya sana,akuna dhambi mbaya kama kumwambia mfalme kuwa umevaa suti umependeza wakati ukijua wakuwa mfalme yuko huchi jambo hilo ni hatari na nilaana” alisema Mbowe.
Mbowe amesema wametumia kila njia,kwa kutumia vyombo vya habari,tumetumia mazungumzo kwa kumshauri Magufuli lakini ametia pamba masikioni na badala yake amekuwa hataki kusikia jambo lolote kutokana na kutaka kufanya utawala wa kiubame.
“Nataka kuwaeleza watanzania pamoja na Rais Magufuli kuwa vitendo vyake vimewaumiza watanzania zaidi ya milioni 50 kutokana na hali hiyo nchi haiku sala,kidemokrasia ,kiuchumi na kibiashara” ameeleza Mbowe.
Mchanga wa dhahabu.
Katika ufunguzi huo mbowe amesema watanzania wanatakiwa kuwa kinachofanywa na serikali ni usanii mtupu kwani serikali ya CCM imekuwa ikiruhusu wizi wa madini na kuaza kupiga kelele yenyewe jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wa nchi.
Amesema Chadema imekaa na kamati kuu pamoja na wataalamu mbalimbali na kupokea taarifa mbalimbali kwa kuangalia propaganda ya mchanga wa dhahabu ambao umekuwa ukipigiwa debe kwa maelezo kuwa serikali imeokoa matrioni ya hela jambo ambalo ni usanii.
Amesema suala zima la kuwepo kwa wizi au kupata hasara kutokana na kuibiwa kwa madini kunatokana na sera mbovu za madini ambazo zinapitishwa na bunge kutokana na kupitishwa na wabunge wengi ambao ni kutoka CCM.
Amesema suala la madini ni kutokana na mikataba mibovu ambayo serikali ya CCM imekuwa ikiingia na hata hivyo mchanga wa dhahabu uliokamatwa bandarini si wa kwetu kimkataba bali ni mali yao hao wawekezaji na kilicho mali ya Tanzania ni asilimia nne tu ya mapato yote.
Hata hivyo alisema mgodi wa Bulyankulu na buzwagi ni kati ya migodi ambayo haina mashine za kuchenjua madini kutokana na kuwa migodi hiyo inazalisha madini zaidi ya dhahabu.
Amesema kutokana na kutokuwa na mashine ya kuchenjua dhaabu ambayo uzalishwa zaidi ya moja wanalazimika kupeleka mchanga nje ya nchi kwa maelezo kuwa kuleta mashinne nchini ni gharama kubwa.
Pamoja na hayo alisema kabla ya mchanga kupelekwa nje ni lazima taasisi mbalimbali na mamlaka kama vile,GST,TRA na TMAA wanalazimika kufanya utafiti wa kinachosafirishwa na kama hawakufanya hivyo inakuwa ni uzembe wa taasisi hizo za serikali.
Mbali na hilo Mbowe alisema serikali kupitia kwa Rais Magufuli imekuwa ikiwaaminisha watanzania kuwa wameokoa matrioni ya hela bila kujua kuwa kisheria bado Tanzania inapata asilimia 4 tu ya mauzo ambayo yanapatikana kutokana na madini ambayo yanapatikana hapa nchini jambo ambalo ni hatari zaidi.
Taswira ya Hali ya uwekezaji.
Mbowe amesema kwa sasa hali ya uwekezaji inazidi kuwa mbaya kutokana na kilichofanyika cha kuzuia mchanga wa dhaabu kutokana na kukiuka mikataba ambayo zaidi ya miaka 15 sasa imekuwa mibovu na imekuwa ikipigiwa kelele na chadema ibadirishwe lakini serikali ya CCM imekuwa ikiziba masikio.
Amesema mikataba mibovu siyo migeni kwa serikali ya CCM kwani ilianza wakati wa ubinafsishaji wakati wa Benjamini Mkapa akiwa rais, akafuatia Rais Kikwete na wakati huo Rais Magufuli alikuwa mmoja wa baraza la mawaziri.
Amesema kwa sasa taswira ya uwekezaji inazidi kuwa mbaya kwani wawekezaji katika gesi asilia pamoja na uchimbaji wa mafuta wanaaza kuondoka na wengine sasa wanapungua jambo ambalo ni bay asana kwa uchumi wa taifa.
Mahusiano ya Rail Odinga.
Baraza kuu la chadema limetoa msimamo wa kutokuwa wasirika wa kutomuunga mkono Raila Odindi kwa kile ambacho wanakieleza kuwa aliwasaliti wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 badala ya kuwaunga mkono chadema alimuunga mkono Magufuli.
Kutokana na hali hiyo Mbowe amesema kwa sasa Chadema wameamua kumuunga mkono Uhuru Kinyatta kwa madai kuwa tangu amekuwa rais wa Kenya amekuwa akisimamia demokrasia na hajawahi kukanyaga na kuvunja sheria za nchi.
Hali ya uchumi
Kiongozi huyo alisema kwa sasa uchumi wan chi umeshuka sana huku deni la taifa likiendelea kupaa hadi kufikia trioni 49 huku wananchi wakiendelea kuwa na hali mbaya ya kiuchumi .
Aidha alisema serikali inashindwa kutekeleza bajeti yake kutokana na serikali kutokuwa na fedha za kujiendeleza katika maendeleo kutokana na kuendelea kusubiria misaada kutoka nje jambo ambalo ni hatari zaidi.
Kufukuza watumishi.
Amesema hatua ya Rais Magufuli kuwafukuza watumishi zaidi ya 10,000 huku akitangaza kutowalipa mishahara yao ni kutengeneza kuchi na kutaka kuwaua watu pasipokuwa na sababu.
Mbowe amesema kama kweli Magufuli ana nia ya kuwafukuza watu wenye vyeti feki huku akijua wazi kuwa wapo watu ambao wanakaribia kustaafu ni kwanini ameendelea kumkubatia mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambaye anajulikana wazi kuwa vyeti vyake havipo hata katika baraza la mitihani.
“Kawatumibua watu ambao walikuwa kazini kwa muda mrefu sana na wengine wanakaribia kustaafu,tena anatumia ubabe na kulazimisha watu wasilipwe mishahara yao,utafiti wa miezi mine umesababisha watu zaidi ya 10,000 kufukuzwa kazi wakati wapo watu ambao walikuwa wana bifu zao wameoneana hakuweza kufanya utafiti wa kujiridhisha jambo hilo ni uonevu mkubwa na wa hali ya juu” ameeleza Mbowe.
Ujenzi wa chama
Kutokana na maelezo ya mbowe aliwataka viongozi wa Chadema sasa kutumia ubabe na udikiteta unaofanywa na rais Magufuli kuwa ni fursa pekee ya ujenzi wa chama ikiwa ni pamoja na kuingia katika mapambano yasiyokuwa na uoga.
Aidha amesema kwa sasa chadema kutokana na kukua kwa kasi na kuelekea kushika dola kwa sasa wamebadilisha mfumo wa vikao vyao vya baraza kuu na kuanza kufanya vikao kwa mfumo wa serikali kwa maana ya kufanya vikao vya kutathimini kazi zao na bajeti ya chama kama ulivyo mwaka wa serikali tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Amesema baraza kuu la Chadema taifa ni kikao cha kawaida cha kikatiba kwa kutafakari kazi kujadili bajeti na kulidhia bajeti na kueleza kuwa awali mikutano hiyo ilikuwa ikifanyika Januari hadi Machi,lakini kutokana na kukua kwa chama na kuelekea kushika dora wamebadilisha na kuanza kufanya vikao vyao katika mwaka wa serikali ili kujenga tabia ya kufanya kazi kiserikali serikali.
Lowassa apokelewa kifalme
Wakati huo huo waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa ameshangiliwa na umati mkubwa wa baraza la Chadema Taifa aliposimama na kuanza kuimba wimbo wa kuwahamasisha vijana,viongozi,wabunge na wajumbe wa baraza juu ya wimbo uliokuwa ukiimbwa hivi.
“Chadema msilale,lalelale Chadema Msilale bado mapambano”