Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:07 pm

NEWS: BANK YA DUNIA YASITISHA KUPIGA KURA KUAMUA MKOPO WA TANZANIA $500M

Benki ya Dunia imeahirisha kupiga kura kuhusu mkopo wa Takribani dola za kimarekani milioni 500 kwa Tanzania zilizokuwa zikilenga miradi mbalimbali ya kielimu.

Kura hiyo ilikuwa inatarajiwa kupigwa mchana wa leo lakini tayari kulikuwa na mgawanyiko mkubwa wa maoni ya wajumbe juu ya benki hiyo iidhinishe mkopo huo kwa Tanzania ama la.

Image result for world bank committee 2020"

Taarifa za kuahirishwa kwa kura hiyo imekuja siku chache baada ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati wa Tanzania na wa kimataifa waliokuwa wakiitaka benki hiyo isitoe mkopo huo kwa serikali kutokana na kile walichokiita kuwa ni sera na sheria ya elimu ya kibaguzi.

Kwa mujibu wa nyaraka za Benki ya Dunia, pamoja na mambo mengine, mkopo huu ulikusudiwa kwenda kusaidia upatikanaji wa elimu bora na kwa urahisi kwa wanafunzi waliokuwa wanarudi shule baada ya kuwa wamepata ujauzito.

Image result for world bank committee 2020"

Kipengele ndicho kinachozua utata kiliwasukuma wanaharakati wa Tanzania kuiandikia bodi ya utendaji ya Benki ya Dunia ikiwa benki hiyo itaipa Tanzania mkopo huo, kabla ya nchi hiyo haijaahidi kuondoa sera na kipengele cha sheria kinachowakataza wanafunzi wa kike kurudi shuleni baada ya kujifungua, basi benki itakuwa imekubaliana na sera na sheria hiyo ambayo wanaharakati wanaiita ya kibaguzi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN la nchini Marekani, limeripoti kuwa hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu kuahirishwa kwa kura hiyo japo inaripotiwa kuwa uongozi wa benki hiyo ulifanya kikao cha dharura na wanaharakati wa haki za binaadamu kutoka Tanzania na mashirika ya kimataifa jana Jumatatu.

Sheria ya elimu ya Tanzania imebeba kipengele za nidhamu ambacho kinaipa mamlaka uwezo wa kuwafukuza shuleni wasichana wanafunzi wanaogundulika kuwa na ujauzito.