Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 6:33 pm

NEWS: BANK KUU YAZITANDIKA FAINI BENKI 5 NCHINI

Dar es salaam: Benki kuu ya Tanzania (BoT) imezipiga faini benki tano za nchini hapa kutokana na kukiuka kanuni namba 17, 20 na 28 za sheria inayozuia utakatishaji wa fedha haramu ya mwaka 2012.

Tokeo la picha la bot tanzania

Benki zenyewe zilizopigwa faini ni pamoja na benki ya Equity Bank (Tanzania) Sh580 milioni, African Banking Corporation Sh145 milioni, Benki ya I&M Bank (Tanzania) Sh655 milioni, Benki ya UBL Tanzania Sh325 milioni na Benki ya Habib African Sh175 milioni.

Tokeo la picha la EUITY BANK

kwamujibu wa Taarifa iliyotolewa na BoT mnamo Septemba 19, 2019 imeeleza kuwa benki hizo zitapaswa kuhakikisha zinarekebisha kasoro zilizobainika ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu kutolewa kwa adhabu hiyo.

BoT imesema benki hizo zilishindwa kuhakiki taarifa za utambulisho wa wateja na kushindwa kuwasilisha taarifa ya miamala yenye kuleta mashaka katika Kitengo cha Kuzuia Fedha Haramu (FIU).

Benki hizo zimetakiwa kupitia upya taarifa za wateja wao na kuhakikisha kwamba zinakidhi matakwa ya kisheria na kanuni zilizopo za uhakiki wa utambulisho wa wateja (KYC) na Kuwasilisha taarifa ya miamala yenye kuleta mashaka ambayo ilitakiwa kuwasilishwa FIU.

Pia kufanya tathmini ya ubora wa mifumo ya ndani ya kibenki na kuchukua hatua stahiki kuhakikisha mifumo hiyo ipo madhubuti kwa lengo la kukinga mapungufu hayo hayarudii tena na Kuwachukulia hatua stahili wafanyakazi wote waliohusika kufanikisha ufunguaji wa akaunti za amana kinyume na kanuni za kumtambua mteja (KYC).