- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: BAADA YA SPIKA KUMTUHUMU ZITTO KWA UTORO, ZITTO AMEMJIBU HAYA
Kigoma: Mbunge wa kigoma Ujiji Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa yeye hajatoroka bungeni kama alivyoripoti spika wa bunge Job Ndugai ila yupo jimboni kwake kukamilisha miradi ya maendeleo ili kusaidia jimbo lake la kigoma Ujiji, akijibu swali aliloulizwa na kituo cha habari cha Azam Tv jana kupitia Akaunti ya Twitter, kuwa kunataarifa kutoka kwa spika wa bunge Job Ndugai zinazodai kuwa unatoroka Bungeni . Je, wewe unasemaje , "kwa sasa ninamajukumu mengi ya Miradi ya maendeleo kusaidia kigoma ujiji, ndio maana sipo Dodoma. Sijatoroka na si peke yangu ambaye sipo" alimalizia Zitto
Mikwaruzano hiyo imekuja baada ya Zitto kumtuhumu Spika wa bunge Job Ndugai kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa muhimili wa bunge Unatumiwa na serekali na pia aliandika kuwa Hatujawahi kuwa na Spika anayedhalilishwa Na Rais,na kwamba Spika alimuuliza Rais wajumbe gani awaweke Kamati za uchunguzi za Bunge?. kitu ambacho zitto anaona si sawa kwa sababu ya kila muhimili unajitegemea kimajukumu na kimaamuziZitto alisema anaona kuwa Spika ameibui swala lake ili kufunika sakata la Mh Tundu Lissu la kupigwa Risasi wananchi wasilifuatilia, kitu ambacho ameonesha kuwa hata kuwa tayari juu ya mpango huo "Nimegundua Spika Ndugai ameibua mashtaka yangu ili kufunika ufuatiliaji wa wananchi kuhusu Lissu kupigwa risasi. Nimeamua sitawapa hilo."