- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AUAWA KWA KUKATWA SHINGO NA KICHWA KUCHOMWA MOTO
DODOMA: MTU mmoja Mariam Said mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mkazi wa Kigoma ambaye alikuwa akiishi kitongoji cha Chang’ombe kilichopo kijiji cha Chamwino Ikulu wilayani Chamwino mkoani hapa ameuawa kikatili kwa kukatwa shingo na kutenganishwa na kiwiliwili chake.
Tukio hilo limetokea leo saa kumi usiku pia iadaiwa kichwa chake kilichomwa moto ikiwemo kuchomwa sehemu za siri pamoja na sehemu mbalimbali za mwili wake.
Akielezea tukio hilo leo Mjini Dodoma,Kamishna msaidizi mwandamizi wa Jeshi la Polisi,Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, LAZARO MAMBOSASA amesema kuwa tukio hilo limetokea Agosti 8 mwaka huu mnamo majira ya saa 4 usiku katika kijiji hicho cha Chamwino ikulu.
Aidha Kamanda MAMBOSASA amebainisha kuwa kutokana na tukio hilo,Jeshi la Polisi Mkoani humo linawashikilia watu 11 kwa uchunguzi kutokana na mauaji hayo.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wa kijiji hicho kuikataa fedheha hiyo ya washirikina ambapo Jeshi la Polisi wakati linafanya uchunguzi wa tukio hilo kuwafichua wale wote waliohusika kuandaa mpango na kutekeleza mauaji hayo.
Katika tukio jingine mtu mmoja ambaye ni mkazi wa Ntyuka katika Manispaa ya Dodoma MASUMBUKO NYERERE mwenye umri wa miaka 24 mkulima amefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi cha mchanga wakati alipokuwa anachimba mchanga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma,LAZARO MAMBOSASA amesema kuwa tukio hilo limetokea Agosti 8 mwaka huu mnamo majira ya saa moja asubuhi katika kijiji hicho.