- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ASKOFU PENGO ARUHUSIWA KUJIUZULU WADHIFA WAKE
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ameridhia ombi la Kiongozi wa Jimbo Kuu Katoliki la DSM Kardinali Polycarp Pengo la kustaafu majukumu ya kuliongoza Jimbo Kuu la DSM.
Nafasi Pengo imechukuliwa na Askofu Mkuu mwandamizi, Yuda Ruwa’ichi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Charles Kilima, Askofu Pengo ameng’atuka baada ya kuomba kustaafu majukumu ya kuliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaam ombi lililoridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko na kumteua Askofu Ruwa’ichi kushika nafasi hiyo.
Katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Miaka 75 ya kuzaliwa kwake, Askofu Pengo aliwaambia waumini wa Jimbo kuu la Dar es Salaam kwamba, anasubiria wakati wowote kumtii Baba Mtakatifu Francisko atakapomwambia kupumzika katika utume wa Kiaskofu.
Askofu Pengo ameliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa miaka 27 tangu mwaka 1992 akimpokea Askofu Laurean Rugambwa.