- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ASKOFU BAGONZA " WALIOPITA BILA KUPINGWA HAWANA FURAHA"
Arusha. Askofu wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Benson Bagonza amesema watu wote walioshiriki na ambao hawakushiriki na waliosusia Uchaguzi pamoja na waliokaa kimya kwenye uchaguzi wa Serekali za Mitaa nchini Tanzania uliofanyika jana Novemba 24, 2019 hawana furaha wakiwemo wasimamizi wa Uchaguzi, Waliopita bila Kupingwa, waliosusia uchaguzi na waliotangazwa wameshinda.
Dkt Bagonza ameyataja makundi takribani 14 ya watu anaodai hawana furaha kutokana na uchaguzi wa jana.
Askofu Bagonza ametoa andiko jipya leo Jumatatu Novemba 25, 2019, ikiwa ni siku moja baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo ambao kwa sehemu kubwa wagombea wa chama tawala CCM wamepita bila kupingwa maeneo mengi.
Katika andiko lake hilo ambalo linasambaa katika mitandao ya kijamii ikiwamo makundi ya WhatsApp, Askofu Bagonza anasema waliopiga kura hawana furaha na waliosusa au kususwa hawana furaha.
Anasema waliopita bila kupingwa nao hawana furaha, waliosimamia kura hawana furaha, walioshinda hawana furaha na hata walioshindwa hawana pia furaha na uchaguzi huo.
Katika andiko hilo, Askofu Bagonza anasema waliopanga yaliyotokea hawana furaha, waliopangiwa yaliyotokea hawana furaha na walioshauri hekima hawana furaha.
Anasema kutokana na uchaguzi huo, waliokaa kimya hawana furaha, wanaounga mkono nilichoandika hapa hawana furaha na wanaopinga anachoandika hapa, hawana furaha. “Wanaodhani wana furaha pia hawana furaha. wapinzani hawana furaha, wapinzani wa wapinzani, hawana furaha.
Wanaodhani hawana furaha ni kweli hawana furaha na kuhoji furaha yuko wapi,” anasema Uchaguzi wa serikali za mitaa umefanyika jana Jumapili huku vyama sita vya upinzani vikisusia uchagizi huo ambavyo ni Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, UPDP, Chaumma na ACT- Wazalendo.