- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ASKOFU ATAKA UCHAGUZI WA SEREKALI ZA MITAA KUHAIRISHWA
Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Owdenburg Mdegela ameitaka Serekali ya Tanzania kuhairisha uchaguzi wa Serekali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu kwasababu ya kutokuwepo na Uwakilishi wa vyama vya upinzani katika uchaguzi huo.
“Kwa nini wasiahirishe uchaguzi kwanza ili mambo ya siasa yakae sawa? Kujiondoa kwa upinzani mimi nimehuzunika, sikufurahia kabisa kwa sababu tunahitaji upinzani ili mambo yakae sawa. “Kwa kazi nzuri aliyoifanya Rais Magufuli (John) hili jambo linaweza kuleta doa. Pamoja na ukorofi wa wapinzani bado wanatakiwa kupewa nafasi ya kuingia kwenye uchaguzi,” amesema askofu huyo
Askofu Mdegele amesema ni vizuri kwa wanasiasa kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kupata suluhisho linaloweza kusaidia vyama hivyo kuingia kwenye chaguzi.
Askofu Mdegela ametoa maoni hayo ikiwa ni siku kadhaa baada ya vyama kadhaa vya upinzani vikiwemo Chadema na ACT- Wazalendo na leo hii NCCR Mageuzi kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa madai ya kutokuridhika na mchakato huo.
Alionya nchi kwa sasa ikikosa upinzani itasababisha matatizo kidogo na ikiendelea hivi mwakani italeta doa kwenye uchaguzi waU- rais na wabunge