- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ASKOFU APINGA USHOGA NA MISAADA YAKE
DODOMA: ASKOFU mkuu wa Kanisa la Anglikana la Kiinjili Jimbo la Tanzania,Ainea Kusenha amekemea vikali baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa wakiunga mkono ushoga au kupokea misaada kutoka kwa watu wenye imani ya kuamini kuwa ushoga ni jambo sahihi.
Mbali na hilo Askofu Kusena amesema migogoro mingi ndani ya imani inatokana na viongozi wa dini kutomuheshimu Mungu wanayemtumikia na badala yake wanageuza sehemu zao wanazoziongoza kuwa ni sehemu ya kujinufahisha kwa kufuja mali zilizopo.
Kiongozi huyo wa Kiroho alitoa kauli hiyo wakati wa Ibada maalum ya kumweka wakfu Wakili Msomi Kuwayawaya .S.Kuwayawaya kuwa askofu msaidizi Dayosisi ya Dodoma,na ibada hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Iringa Mvumi.
Akihubiri katika ibada hiyo alisema kwa sasa makanisa mengi,Dayosisi,nyumba za uaskofu pamoja na madhehebu mbalimbali yanaparanganyika kutokana na viongozi kuwa na tamaa ya mali na badala ya kufanya kazi ya Mungu wanageuza dini kuwa kivuli cha kujinufaisha.
“Wakati mwingine unaweza kuona utoto wa imani vitabu vitakatifu vyote vitakatifu vinaeleza wazi kuwa ndoa ya jinsia moja haifai ni dhambi,lakini unakuta kiongozi amesimama anapokea misaada kutoka kwa watu wenye kujihusisha na ushoga na wakati mwingine anaunga mkono.
“Na haya yote si kwamba viongozi wa dini hawayajui lakini kwa kuwa hawana hofu ya Kimungu ndiyo maana wanafanya hivyo,lakini kibaya zaidi ni pale ambapo viongozi kama vile maaskofu baada ya kukemeana na kukosoana wamekuwa wakilindana.
“Wakati mwingine madhara makubwa yanatokea kusababisha mipasuko kutokana na viongozi wa dini ambao wanachaguliwa kupata nafasi hizo kwa kutoa rushwa ili wachaguliwe jambo ambalo limekuwa kikwazo kikubwa katika utumishi wa Mungu”alisema askofu Kusenha.
Katika hatua nyingine askofu Kusenha aliwataka maasikofu pamoja na viongozi wote wa dini mbalimbali nchini kuheshimu katiba zinazowaongoza na kuachana na tabia ya kuwa na kiburi pindi wawapo katika utumishi wa Mungu.
Kanisa Anglikana la kiinjili Jimbo la Dodoma ni kanisa ambalo limeanzishwa na askofu Mkuu wa sasa Ainea Kusenhamiaka 8 sasa kutoka kanisa Angilikana kutokana na mgogoro wa pande mbili kwa viongozi na waumini ambayo upande mmoja ulikuwa ukipinga ushoga na upokeaji wa misaada kutoka kwa mashoga na upande mwingine ulikuwa ukikubalina na ushoga na misaada kutoka kwa mashoga.
Naye askofu msaidizi wa Dayosisi ya Dodoma Kuwayawaya S Kuwayawaya mara baada ya kusimikwa kuwa askofu akitoa salamu zake za shukrani kwa viongozi wa dini na wahumini alisema katika utumishi wake ataendelea na mapambano ya kupinga ushoga na kutopokea misaada inayotolewa na watu wanaoamini ushoga kuwa siyo dhambi.
Pia alisema ataendelea kuhubiri amani huku akikemea utawala wa mabavu ambao unaweza kuhatarisha usalama na amani ya nchi na kudai kuwa mahali popote vi vyema kuzingatia misingi ya kikatiba na sheria zinazoongoza sehemu husika.
“Napenda nimshukuru Mungu sana lakini pia ni seme katika utumishi wangu Nitapinga Ushoga kwa nguvu zote,uonevu,nitakemea uvunjwaji wa katiba na sheria kwa viongozi,vitendo vya rushwa,lakini kanisa litatakiwa kujihusisha katika shughuli za maendeleo ya jamii.
“Pia nampongeza rais wa awamu ya Tano Dk.John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya lakini pia wasaidizi wake wanatakiwa kumshauri vyema mkuu wan chi kwa njia yoyote kwani hata matamko ya rais yanapotolewa yasiweze kuwa na ushahidi au kutolewa ushahidi licha ya kuwa yanaweza kutokubaliwa na mtu mwingine” alisema Kuwayawaya.