Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:41 am

NEWS: ASKOFU AMTAKA RAIS MAGUFULI KUWAPA UHURU WATU KUZUNGUMZA

Dar es Salaam: Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Amani Lyimo amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kuwapa uhuru wananchi kuzungumza na kusema maswala mbali mbali inapowezekana kwa sababu kufanya hivyo ndiyo demokrasia.

Mch. Lyimo ametoa kauli hiyo leo Jumatano Januari 23, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam katika mazungumzo kati ya Rais Magufuli na viongozi mbalimbali wa madhehebu ya kidini hapa nchini.

"Suala la demokrasia Mheshimiwa Rais, watu wana hofu hata kama huambiwi na watendaji wako, ila jua watu wanahofu, kama kazi baba unapiga kweli wewe waachie wazungumze maana Watanzania hawatachagua maneno bali watachagua kazi, wape uhuru waseme"- Mchungaji Lyimo

Amesema Watanzania wengi wanahofu hata kama haambiwi na watendaji wake ila wengi hawathubutu kuzungumza licha ya kuwa anafanya mambo mengi mazuri. “Kwa kazi unayoifanya watu hawatachagua maneno bali watachagua kazi, kwa hiyo kama kuna uwezekano waachie pumzi kidogo wazungumze lakini hawatakushinda kwa maneno yao,” amesema Lyimo.