Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:59 am

News: ASKOFU ahoji nini kinacho endelea kati ya Rais Magufuli na RC Makonda

Dodoma: ASKOFU wa Kanisa la Gosple Ministry (GMC), Christopher Madole, amehoji kinachoendelea kati ya Rais Dk.John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,( …), kiasi cha kusababisha tuhuma dhidi ya RC huyo kupuuzwa huku usalama wa wananchi, ukianza kuhofiwa.

Akihubiri kanisani hapo katika semina ya kiroho, Askofu Madole, amemzungumzia matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea nchini, ikiwamo baadhi ya wananchi kutekwa na kurejeshwa wakiwa wamejeruhiwa huku wengine wakiendelea kutofahamika waliko.

Amerejea malalamiko ya baadhi ya wabunge, wengi wakiwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwamba upo mpango wa kuwateka wabunge 11 kwasababu mbalimbali, akisema kupuuza malalamiko hayo na kutumia itikadi za kisiasa kuwanyamazisha, ni kukumbatia uhalifu na kuhatarisha usalama wa taifa.

“Tunaofatilia na kutafakari bila kufungamana na upande wowote, tunajiuliza hawa watumishi wetu wa usalama wa taifa wako wapi? Hata viongozi wa dini ambao wanakaa kimya huku wakishuhudia wananchi wakitoa vilio kwa njia tofauti, inabidi wabadilike, watimize majukumu yao,” amesema.

Alisema ni dhahiri wanaoteka wananchi ni miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali, hivyo viongozi wa kiroho kubaki kimya ni unafiki na alimpongeza Askofu Josephat Gwajima, kwa namna anavyokemea maovu yanayoibuka katika jamii na taarifa kumfikia.

Akimzungumzia RC wa Dar es Salaam, Askofu Madole, aliitaka taasisi ya rais ambayo ndiyo kubwa kuliko zote, ifanye utafiti na kuchukua hatua dhidi ya tuhuma zote zinazomkabili kiongozi huyo wa mkoa ili jamii irejee katika hali ya utulivu kisaikolojia.

Pia ametaka wateule wote wa Rais, kuacha uwoga badala yake, waseme ukweli ili kumsaidia aliyewateua katika kuiendesha nchi.