Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:55 am

NEWS: ASKARI APANDISHWA KIZIMBANI KWA MAUAJI

DAR ES SALAAM: ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Marwa Wambura (25) amepandishwa kizimba Katika Mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kuua.


Akisomewa mashitaka hayo kwa mara ya kwanza katika Mahakama hiyo, mbele ya hakimu Isic Kuppa, mwendesha mashitaka Joseph Nasua alidai kuwa Juni 17, 2017, maeneo ya Kibamba CCM, wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, mtuhumiwa Rashid Sadick alitenda kosa hilo huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza shitaka hilo.