- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ASKARI 6 WALIOIBA MAFUTA YA NDEGE WAHUKUMIWA KULIPA LAKI 5
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewahukumu askari sita akiwemo mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kulipa faini ya Sh500,000 kila mmoja baada ya kukiri shtaka lao la wizi wa mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik).
Askari hao ni nipamoja na askari wa JWTZ, MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47) na askari polisi, Koplo Shwahiba (38), Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson na PC Hamza.
Hukumu hiyo ilitolewa jana Ijumaa Oktoba 4, 2019 na Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo baada ya washtakiwa hao kukiri shtaka linalowakabili.
Mwaikambo alisema kwa kuwa washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza hivyo mahakama hiyo imewapa adhabu ya kulipa faini ya Sh500, 000 kila mmoja na inawataka kulipa thamani ya zaidi ya Sh4 milioni ya mafuta ya ndege yaliyoibiwa na lita 109 zenye mafuta hayo yatarudishwa serikalini.
Awali, wakili wa Serikali Mwandamizi Renatus Mkude aliieleza mahakama hiyo kuna utaratibu wamekubaliana ili kumaliza shauri hilo.
Alidai kuwa awali washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na makosa matatu hivyo walikubaliana kuliondoa shtaka la kwanza la kupanga genge la uhalifu na shtaka la tatu ni la utakatishaji wa fedha na shtaka la pili la wizi limebaki.
Washtakiwa hao wanadaiwa Julai 30, 2019 katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik) yenye thamani ya Sh4.64 milioni mali ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambayo waliyaweka kwenye madumu 109 ambalo wote walikiri.