- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ASKARI 4 WASIMAMISHWA KAZI KENYA KWA UNYANYASAJI
Serikali ya Kenya inajaribu kijisafisha kwenye macho ya kimataifa mara baada ya leo kuchukua hatua dhidi ya mauaji na ukatili unaoripotiwa kuendelezwa na maafisa wa polisi wanapotekeleza amri ya kutotoka nje ya saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi.
Idara ya usalama imetangaza kuwa polisi wanne wamesimamishwa kazi kusubiri uchunguzi.
Haya yanajiri huku watu wawili zaidi wakiripotiwa kuwaua katika maeneo ya Kakamega na Kwale.
Marcus Ocholla, kamanda wa polisi mkoani bonde la ufa amethibitisha kupokea ripoti kadhaa kuhusu maafisa wa polisi kuwajeruhi raia.
Katika muda wa wiki moja sasa, kumekuwa na ongezeko la matukio ya maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na wakenya wanaopatikana nje baada ya kuanza kwa muda wa marufuku ya kutembea usiku.
Hapo jana watu wawili zaidi waliripotiwa kuwaua huko Kakamega na Kwale.