Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:44 am

NEWS: ASILIMIA 29 YA VIJANA HAWANA AJIRA

DODOMA: SERIKALI imesema asilimia 56 ya vijana nchini wanauwezo wa kufanya kazi ikiwemo mjini na vijijini na asilimia 29 wanaukosefu wa ajira.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama wakati wa maadhimisho ya vijana Duniani yaliyofanyika leo mjini hapa.

Amesema asilimia 79.9 ya vijana wenye kiwango cha chini cha nguvu kazi ikiwemo asilimia 18 ya vijana wa mjini wanaukosefu wa ajira.

"Kiwango cha chini cha vijana wenye ukosefu wa nguvu kazi SERIKALI imejipanga kudhatiti kukuza nguvu ya vijana nchini" amesema Mhagama.

Mhagama amesema mimba za utotoni ni moja ya changamoto inayosababisha kupunguza nguvu kazi ya vijana katika harakati za kupambana na kuleta maendeleo nchini.

Amesema SERIKALI imeandaa ''programu'' ya ujunzi kwa vijana ili kukuza uchumi wa taifa.

"Nawaomba wakurungezi wote kutenga asilimia 5 kwa ajiri ya vijana" amesema mhagama.

"Ninawaomba vijana wote kwenda katika ofisi za kilimo ili kuuliza jinsi ya kuratibu kilimo cha utalu nyumba." Amesema mhagama

Kwa upande Katibu wa Mkurungezi mtendaji [MD] salama foundation shadrack Msuya amesema maadhimio ya vijana ni kuiomba SERIKALI kuboresha utawala bora,kukuza na kuimarisha vyombo vya habari utasaidia kukuza uchumi wa Tanzania.

"Naviomba vyombo vya Habari kuzingatia weledi katika utendaji kazi na kuanda midahalo ambayo itasaidia kuwahamasisha vijana katika kulinda amani ya nchini." Amesema Msuya.

Pia amesema anaiomba serikali kuongeza jitihada za kupambana na madawa ya kulevya ili kuendelea kudumisha amani.

Maadhimisho ya vijana duniani yalianza kufanyika mwaka 2000 na huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 mwezi wa nane.