Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 11:34 pm

NEWS: APIGILIWA MISUMARI MIKONONI NA WATU WASIOJUILIKANA

Katika hali ya Kusikitisha Kijana Mmoja Jina Kasumba Baker mwenye umri wa miaka 21, mkazi wa Kawempe nchini Uganda, amevamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa vibaya maeneo ya kichwani, kisha kupigiliwa misumari miwili kwenye mikono yake yote miwili.

Baada ya tukio hilo Upinzani nao nchini Uganda wanamtuhumu Rais Yuweri Museveni kwa kutekeleza Ukatili huo.

"If this is true, we condemn it in the strongest terms. KagutaMuseveni & his regime got power by using extreme violence on our people & have sustained themselves in power through extreme violence" aliandika Bobi wine Mbunge wa Upinzani

Taarifa za awali zimeshindwa kudhibitisha kwamba ni nani hasa anaweza kufanya ukatili huo.

Polisi nchini humo imetoa taarifa yake jana kuwa wanaendelea kufalifanyia uchunguzi tukio hilo la unyama dhidi ya kijana huyo.

Nchini Uganda kwa miaka ya hivi karibu kumekuwepo na vitendo vya watu kufanyiwa ukatili na wengine kukutwa wameshafariki tayari.

Mwezi jana mshika wa mwana muziki nchini Uganda Bob Waine alikuwa alikutwa ameuwawa na watu wasio julikana .

Mashirika ya Haki za kibinaadamu nchini Uganda yamekuwa yakipiga kelele kwa muda sasa juu ya kutokea kwa matukio yanayokiuka haki za kibinaadamu nchini humo ambayo kimsingi wanaona kama yanahatarisha usalama wa watu wa nchi hiyo.