- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ALIYEPANGA KUMUUA NAIBU RAIS WA KENYA (RUTTO) AKIRI MAHAKAMANI
Mahakama ya mjini Nairobi imeamuru kuendelee kushikiliwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kidijitali katika ikulu ya Kenya, Dennis Itumbi katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga ili kuruhusu polisi kuchunguza madai makubwa aliyoibua mkurungezi huyo.
Kabla mahakama ya Nairobi haijatoa uamuzi, Itumbi alimwambia hakimu kuwa ni kweli kulikuwa na mkutano uliofanyika katika hoteli ya La Mada ambao agenda yake ilikuwa ni kumuua Ruto.
Itumbi alimwambia hakimu kuwa alikuwa na video kuthibitisha madai yake na kuiomba mahakama aionyeshe lakini hakimu hakutoa neno kama aonyeshe video hiyo.
Itumbi alisema alipeleka taarifa hizo hizo kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai lakini polisi wameonyesha wana nia na yeye kufikishwa mahakamani na si kuangalia ukweli.
Baada ya kusema hayo mahakama iliamuru aendelee kushikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Muthaiga ili kuruhusu polisi kuchunguza masuala makubwa aliyoibua.
Itumbi alikamatwa juzi na polisi kuhusiana na barua ya njama ya kumuua Naibu Rais, William Ruto sasa kubaki rumande kwa siku tano zaidi.
Alimatwa Jumatano Nairobi wakati akipata chakula cha mchana na huenda akashtakiwa kwa kuchapisha taarifa za kutishia.
Wabunge wengi walifika mahakamani jana kwa ajili ya kumuunga mkono Itumbi wakisema wanataka waziri na Katibu Mkuu ambao hawakuwataja kwa majina wachunguzwe juu ya tuhuma hizo za mipango ya mauaji.
Itumbi anashtakiwa kwa kuweka barua hiyo kwenye kundi la WhatsApp la Tangatanga linalomuunga mkono Rutto
Uchunguzi wa awali kuhusiana na barua hiyo umebaini kuwa tuhuma kwamba mawaziri wanne walikutana kupanga njama za kumuua Ruto, si tu kwamba ni uongo lakini pia barua hiyo iliandikwa na watu wa karibu na Ruto.