Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:02 am

NEWS: ALIYEMUUA MKEWE KWA KUMCHOMA MOTO AFIKISHWA MHAKAMANI

Dar es Salaam. JESHI la polisi limemfikisha mahakamani na kusomewa mashitaka Hamisi Saidi (38) ‘Meshack’ kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma na moto mke wake Naomi Marijani.

Meshack ambaye ni mfanyabiashara na Mkazi wa Gezaulole wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu mchana leo.

Akisoma hati ya mashitaka leo Jumanne Julai 30, 2019 Wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ally Salum amedai mshitakiwa huyo anashitakiwa kwa kosa la mauaji kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Simon amedai Mei 15, 2019 eneo la Gezaulole wilayani Kigamboni alimuua Naomi Marijani huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Amedai bado wanaendelea na upelelezi hivyo anaiomba Mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kutajwa shauri hilo.

Hakimu Salum amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo hivyo mshtakiwa huruhusiwi kujibu chochote