- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ALIYEKUWA KATIBU MKUU CHADEMA AJIUNGA NA CCM
Dar es Salaam. Katibu mkuu mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Vicent Mashinji leo Jumanne Februari 18, 2020 amekihama chama chake cha Chadema na kuamua kutimkia chama Tawala cha CCM na kupokewa na katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho tawala nchini Tanzania, Humphrey Polepole.
Dk Mashinji amejiunga CCM katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba, Katika mwa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni miezi miwili tangu ufanyike mkutano mkuu wa Chadema na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kutompendekeza tena kuwa katibu mkuu wa chama hicho kikubwa cha upinzani.
Katika maelezo yake ya leo, Dk Mashinji amesema, “nimuombe mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kama ataridhia anipe nafasi ya kujiunga na CCM ili niweze kuchangia maendeleo ya nchi yangu.”
Baada ya kueleza hayo, Polepole alimkaribish,“mimi nikuhakikishie kwa niaba ya wakuu wa chama wakiongozwa na ndugu Magufuli nimekupokea rasmi karibu sana CCM.”
Baada ya Mashiji kuhudu nafaisi hiyo ya Katibu mkuu Mbowe hakurudisha tena kwenye nafasi yake na badala yake alimpendekeza mbunge wa Kibamba, John Mnyika kuwa katibu mkuu wa tano wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania, kupigiwa kura na baraza kuu.
Baada ya kukosa nafasi hiyo, Dk Mashinji alieleza masikitiko yake kwamba alitamani kuendelea kuwa katibu mkuu ili aweze kumalizia mipango aliyokuwa nayo, ikiwemo maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020.