Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 12:22 pm

NEWS: ALIYEINGIZA CORONA NCHINI AOMBA RADHI

Mgonjwa wa kwanza aliyepatikana kuwa na virusi vya Corona, nchini Tanzania Isabela Mwampamba (46), amewaomba radhi Watanzania kwa kuzua taharuki kutokana na kuwa mgonjwa wa kwanza na kuwataka kutumia muda huu kuelimishana namna ya kujihadhari virusi hivyo.

Akizungumza kwa njia ya simu moja kwa moja (live) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari ili kujua hali yake Isabela amesema anamshukuru Mungu kwani anaendelea vizuri na amekuwa akijipima homa kila siku.

“Namshukuru Mungu nimehudumiwa vizuri ninatamani kusema naomba msamaha kwa kuwa mgonjwa wa kwanza Tanania, nimeleta taharuki, niko hapa nikiomba msamaha naamini Mungu atatulinda na kutuponya,” amesema.

Aidha, Waziri Mwalimu amesema mtandao wa watu 26 walioshirikiana na mgonjwa huyo wako chini ya uangalizi na vipimo vya sampuli vimeshapelekwa jijini Dar Es Salaam na majibu yatatolewa wakati wowote kuanzia sasa.