- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Aliyefanya mauaji na kutuma video kwenye mtandao wa facebook amejiua mwenyewe.
Marekani: Haki miliki ya picha FACEBOOK Image caption Mahusiano na madeni kwenye mchezo wa kamari yalimsukuma Stephens kutekeleza mauaji
Polisi nchini Marekani wamesema mtu ambaye alifanya mauaji kisha kutuma video ya mauaji hayo katika mtandao wa Facebook amejiua mwenyewe.
Wamesema Steve Stephens alijiua wakati maafisa wa polisi walipolikaribia Gari lake walipokuwa wakimkimbiza takribani kilomita 150 kutoka Cleveland, Ohio, eneo la mauaji yaliyofanyika jumapili.
Picha za video za babu akipigwa risasi zilisalia kwenye mitandao ya kijamii kwa saa mbili bila kuondolewa.
Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg, alieleza maskitiko yake kwa ndugu na akaahidi kuwa kampuni itafanya kila linalowezekana kuzuia jambo kama hilo kuwekwa tena mtandaoni.