- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ALICHOKIONGEA TUNDU LISSU BAADA YASEREKALI KUKIRI KUZUILIWA KWA BOMBADIER
Dar es salaam: Mbunge wa Singida mashariki na Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu amehoji kati yake na Rais Magufuli kuwa ni nani kati yao ni Kibaraka wa Mabepara na adui wa taifa la Tanzania, Lissu amehoji baada ya Taarifa iliyotolewa na serekali jana kupitia Kaimu msemaji mkuu wa serekali Bi Zamaradi kawawa kusema kuwa wapo wanasheria wasio mtakia Rais maguli mema katika utendaji wake, kwa kutaka kumkwamisha, sasa naye Lissu amejibu kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuuliza maswali sita akitaka ufafanuzi kwenye maswala mbalimbali ambayo yamefanywa chini ya Rais Magufuli.
"Aliyeingia mkataba wa ujenzi wa Wazo Hill-Bagamoyo Road na kampuni ya SCEL ni Tundu Lissu au Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli??? , Aliyeuvunja mkataba huo bila kujali sheria na madhara ya kushtakiwa nje ya nchi ni Tundu Lissu au ni John Pombe Magufuli???, .Aliyefanya tushindwe kesi ICSID na kuamriwa kulipa mabilioni haya mwaka 2010 ni Tundu Lissu au ni John Pombe Magufuli???" alihoji Lissu
Pia Lissu alitaka kupata ufafanuzi ya aliyechelewasha kutolipwa kwa deni la taifa " Aliyechelewesha malipo ya deni mpaka limefikia bilioni 87 ni Tundu Lissu au ni John Pombe Magufuli??? .Ambaye amevunja Sheria ya Uhujumu Uchumi na anapaswa kuwajibishwa kijinai, kama akina Daniel Yona na Basil Mramba, ni Tundu Lissu au ni John Pombe Magufuli???"
.''Kutokana na yote haya, nani hasa kati ya Tundu Lissu na John Pombe Magufuli ndiye kibaraka wa mabepari na adui wa taifa letu??? .
Mwenye akili na alete majibu''. aliandika Lissu