- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ALICHOKIONGEA SPIKA BAADA YA LISSU OMBI LAKE KUKATALIWA NA MAHAKAMA
Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema kama watu wangekuwa wanaheshimu na kushirikiana na mamlaka zilizopo ni vigumu mtu huyo kupata matatizo
Kauli hiyo ya spika ameitoa leo Septemba 9, 2019 mjini Dodoma mara baada ya mahakama kuu kanda ya Dar es salaam kukataa maombi ya aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kufungua shauri la maombi ya kutengua uamuzi wa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai wa kuufuta ubunge wake.
"Mambo haya pengine mtayasikia wenyewe huko nje, mimi sitaki kuyasema''
Mambo haya ukiheshimu mamlaka huwezi kupata matatizo haya, haiwezekani, bahati mbaya Spika hawezi jitokeza kila wakati kujibu kila mtu anaenda kwenye mitandao sijui ningeweka wapi sura yangu.
"Hivi kumjulisha Spika kwamba mheshimiwa kuwa mimi sitaweza kuhudhuria bunge hili la 16 kwa kuwa nipo kwenye matibabu unaweza kunipigia simu au kuandika message taarifa utakua umetoa.
"Kwa hiyo mengine yote unafanya isipokua kumwambia Spika mwaka unapita tuu nakuona, mengine yote unaweza kufanya ila kuwasiliana na huyu Spika haiwezekani itafika mahali watu wataruka na wewe tu na usipige kelele umeyataka mwenyewe kwa sababu taaratibu mnazijuaa. Kwa hiyo waheshimiwa wabunge Tukifuata taratibu wala hatutagombana"
Habari ya zile fomu, zile za maaadili ni lazima tujaze ni takwa la katiba hata Mh Mbowe aliniandikia barua aliopokua gerezani mwezi wa 12 kwa mba nipo sehemu ambapo siwezi kujaza zile fomu nipo gerezani Segerea lakini nikitoka ntazijaza kwani kulikuwa kuna ugomvi alivyotoka alijaza lakini husemi , huandiki, huwasiliani wala hufanyi nini, wewe unapuyanga na yako ukitoka una yako"
Hahakama kuu Imesema kuwa Rais huyo wa zamani wa TLS hakupaswa kuwasilisha maombi hayo, alitakiwa kufungua kesi ya kupinga uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo.
Lissu alifungua maombi chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai ambaye amempa mamlaka ya kisheria kumwakilisha, ikiwa ni hatua ya awali kabisa ya kupigania kurudishiwa ubunge wake.
Katika maombi hayo namba 18 ya mwaka 2019, dhidi ya Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Lissu aliomba kibali cha kufungua shauri kupinga taarifa ya Spika ya kukoma kwa ubunge wake na mahakama iteunge taarifa hiyo.
uni 28, 2019, wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge, Spika wa Bunge Job Ndugai alitangaza kukoma kwa ubunge wa Lissu, huku alijitetea kuwa si yeye aliyemvua ubunge bali ni matakwa ya Katiba ya Nchi.
Alitaja sababu za uamuzi huo kuwa ni kutokuhudhuria vikao vya bunge kwa muda mrefu bila kumjulisha Spika kwa maandishi mahali aliko na kutokuja taarifa za mali na madeni kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.