Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:38 am

NEWS: ALICHOKIONGEA MWIGULU BAADA YA KUNUSURIKA KIFO LEO KWENYE AJALI

Dodoma: Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Lameck Nchemba amesema amepata ajali baada ya gari alilokuwa akiendeshwa kugonga punda aliyekuwa akikatisha barabarani na kusababisha

Akizungumza leo Jumatano Februari 13, 2019 katika hospitali ya Mkapa jijini Dodoma anakopatiwa matibabu, Mwigulu ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM),amesema alikuwa akitokea mkoani Iringa kuelekea Mkoa wa Singida kuhudhuria kikao cha kamati ya siasa ya Mkoa huo. “Nilikuwa siangalii mbele kwa kuwa nilikuwa naongea na simu lakini ghafla nilishtushwa na tahadhari ya ajali niliyopewa na dareva wangu,” amesema Mwigulu. “Nilipotazama mbele niliwaona punda watatu wanakatisha barabara na mmoja alifanikiwa kuvuka na kuwagonga wengine wawili.” Ameongeza,

“Nilichosikia ni sauti ya kishindo kikubwa kilichoashiria kuwa tumepata ajali, namshukuru Mungu ni mwema kwa kuwa ametuepusha na kifo.” Amesema baada ya hapo aliona moshi umetanda ndani ya gari hali iliyoashiria gari hilo lingeweza kulipuka lakini wasamaria wema walifika na kuwaokoa na kuwawahisha hospitali ya Benjamin Mkapa.