November 26, 2024, 11:25 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AL BASHIRI ASHTAKIWA KWA MAKOSA YA UFISADI
Aliyekuwa kiongozi wa Sudan Omar al Bashir amefunguliwa mashtaka ya ufisadi miezi miwili baada ya kuondolewa madarakani.
Kwa mujibu wa shirika la habari la nchini Sudan SUNA lililomnukuu mwendesha mashtaka wa serikali, Bashir anakabiliwa na mashtaka ya kuwa na fedha za kigeni, kurundika mali kinyume cha sheria na kutoa amri ya hali ya hatari.
Wachunguzi wamemkuta kiongozi huyo wa zamani na zaidi ya Euro milioni 100. Baada ya kuitawala Sudan kwa muda wa miaka 30, wanajeshi walimwondoa Bashir madarakani baada ya maandamano makubwa yaliyofanyika kwa miezi kadhaa.