- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AKATWA UUME BAADA YA KUMNYIMA MKEWA UNYUMBA
Kampala: Gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda limeripoti kuwa Mwanamume mmoja wilayani Apac nchini Uganda, jina Moses Okot (46) amekatwa uume na mke wake kwa madai ya mke huyo kukosa huduma ya unyumba.
Bw. Okot alisema kuwa siku ya jumapili june 30 ambayo ndio siku ya tukio mke wake Beatrice Acen(35) alirudi nyumbani kwake amelewa chakali na kisha kumkata mme wake uume.
“Niliporudi kutoka kuwinda kama saa 1 usiku, mke wangu hakuepo nyumbani. Binti yangu akanipa chakula na baada ya kula nikaenda kulala. Mke wangu alirudi karibu saa 4 usiku na kufoka nimfungulie,” alisema okot.
“Nilikuwa tayari nimelala usingizi. Nilihisi maumivu kidogo yaliyoniamsha na nilipojikuta chupi yangu imelowana damu,” aliongeza.
Okot aliendelea kusimulia “mke wangu amekuwa anakuja nyumbani amelewa sana. Kama mwanamume nilishindwa kuvumilia hali ile, niliamua kumnyima unyumba nikiamini atajirudi. Amekuwa akidai unyumba.
” Okot na Acen wameishi pamoja kwa zaidi ya miaka 10 na wamepata pamoja watoto watano.
Hata hivyo, mwenyekiti wa Kijiji cha Amin B, amesema wanandoa hao wamekuwa wanagombana mara kwa mara. Amethibitisha kuwa mara kadhaa mwanamke huyo amekuwa akipuuza mahitaji yake ya unyumba.
“Si mara ya kwanza Acen anamuumiza mumewe. Mwaka jana alimvunja mfupa wa bega wakati wanapigana na akakimbia. Shauri lilimalizika katika ofisi yangu na wakarudiana,” alisema.
Okot alipelekwa katika Kituo cha Polisi Olelpek kufungua kesi dhidi ya mkewe na kupelekwa katika hospitali ya Apac anakoendelea na matibabu. Polisi wamesema shauri limefunguliwa na kupewa RB namba SD04/30/06/2019 na amepewa fomu ya polisi ya matibabu.