Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:45 am

NEWS: AKAMATWA KWA KUKUTWA NA MIHURI 56 YA SEREKALI

Mbeya: Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ABRAHAM OBEDI [55] wakala wa bima ya GTM na Mkazi wa Isanga Jijini Mbeya akiwa na mihuri hamsini na sita [56] ya idara mbalimbali za serikali na ofisi binafsi ambayo imeghushiwa na kuhifadhiwa katika ofisi yake ya Stationaries.

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 17:00 jioni huko maeneo ya Mtaa wa Sokoine uliopo Kata na Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kupata taarifa na kisha kufanya msako mkali na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa pamoja na vielelezo.

Baadhi ya mihuri na nyaraka alizokutwa nazo mtuhumiwa ni kama ifuatavyo:-
1. Mhuri wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko Kata ya Ruanda,
2. Mhuri wa Afisa biashara wa Halmashauri ya Mbeya,
3. Access Bank Tawi la Mbeya,
4. Mamlaka ya Mapato Mbeya [TRA]
5. Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini,

Aidha mtuhumiwa alikutwa pia na Kompyuta moja aina ya Accer, Stika za bima, Poss Machine na nyaraka mbalimbali vikiwemo vyeti vya wanafunzi ambao vimeghushiwa. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.