- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AJIUA BAADA YA KUMKUTA MKEWE AKILA CHAKULA CHUMBANI NA MPENZI WAKE
Mtu mmoja jina Njawala Ally (37), mkazi wa kijiji cha Magazini Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma amejiua mwenyewe kwa kunywa dawa pamoja na pombe kali ili afe baada ya kumkuta mkewe ndani ya nyumba ya mpenzi wake wakila chakula kilichoandaliwa na mkeo.
Kwa mujibu wa shemeji ya marehemu bwana Daudi Goliama alisema kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na homa ya kisukari kwa muda mrefu akiwa anatumia dawa pamoja na sindano ambapo alizuiliwa kunywa pombe wakati akiwa anakunywa dawa hizo na madaktari wa hospitali ya peramiho alikokuwa anatibiwa.
Aidha bwana Goliama alidai mke wake marehemu Mariamu Msola baada ya kuona hali ya mumewe alijishikiza kwa kijana aitwaye Beula Mohamedi na kumfanya mpenzi wake huku akijisahau kama anamume wa ndoa.
Tukio hilo lilitokea siku ya mwaka mpya mchana ambapo Mariamu alimwandalia mpenzi wake chakula kizuri wakati huo mumewe aliondoka na kwenda kwa majirani kuzungumza .
Mumewe akiwa na majirani walimweleza mwenzao kuwa mkeo ameelekea kwa mpenzi wake amebeba chakula hali iliyomfanya marehemu kurudi nyumbani kuthibitisha kama yupo au hayupo na kwa kuwa marehemu Alisha kuwa na taarifa ya mahusiano yao ya kimapenzi alimwuliza mkeo na alikataa kuwa hana uhusiano naye .
Marehemu hakumkuta mkeo nyumbani na kuamua kwenda nyumbani kwa mpenzi wa mke wake huyo na kumkuta mkeo na mpenzi wake wakiwa ndani ya nyumba ya mpenzi wake wakila chakula kilichoandaliwa na mkeo huyo na ndipo alipomwuliza mkeo kuwa ulikataa kuwa huna uhusiano na huyo hapa umefika kufanya nini na kusononeka na kisha kurudi nyumbani kunywa dawa pamoja na kunywa pombe kali ili afe.
Baada ya kunywa dawa nyingi za homa za kisukari pamoja na pombe kali alizidiwa huku akitamka bayana heri afe kuliko mambo anayofanyiwa na mkeo huyo na baada ya muda mfupi alifariki dunia.
Kaimu Afisa mtendaji wa kata ya Magazini bwana Ally Manoni alithibitisha kifo cha mtu huyo na kudai kuwa kifo hicho kimesababishwa na marehemu kunywa dawa nyingi za homa ya kisukari pamoja na pombe kali .
Marehemu alizikwa tarehe 2januari mwaka huu katika makaburi ya kijiji cha magazini ambapo ameacha mke na watoto wawili mmoja wa kike darasa la pili na mmoja wa kiume anasoma chekechea shule ya Msingi magazini