Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:37 am

NEWS: AJALI YAUWA WAFANYAKAZI 7 WA AZAM TV NA WATATU KUJERUHIWA

Dar es Salaam. Watu saba wakiwemo wafanyakazi watano wa Shirika la habari la Azam Media wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.

Taarifa kutoka katika shirika hilo la habari zinaeleza kuwa wafanyakazi hao walikuwa katika gari aina ya Coaster na kwamba madereva wawili wa magari hayo nao wamefariki dunia.

Taarifa zinaeleza kuwa watu hao ni waandishi wa habari waliokuwa katika safari ya kikazi, wakielekea Chato mkoani Geita. Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi, Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Tabora.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo gari dogo walilokuwa wamepanda wafanyakazi hao limegongana na lori lililokuwa likitoka Igunga kuelekea Dar es salaam.

Miongoni mwa vifo hivyo ni pamoja na wafanyakazi wa Azam Media, Salim Mhando, Florence Ndibalema, Said Haji, Sylvanus Kasongo na Charles Wandwi, wengine ni dereva na utingo wake ambao majina yao hayajafahamika.

Majeruhi ni Mohamed Mwinshehe, Mohamed Mainde ambao wapo ICU pamoja na Artus Masawe ambaye yake ni nzuri kiasi.