- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AJALI YAJERUHI WATU 18
DAR ES SALAAM: WATU 18 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea saa 10:30 alfajiri katika eneo la Madafu barabara ya Pugu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani alisema ajali hiyo ilihusisha gari namba T 337 BKN Nissan Civilian iliyokuwa inatoka Gongo la Mboto – Mombasa kwenda Kariakoo kupitia Banana.
“Gari hilo liliigonga gari la mchanga namba T 656 DHL Scania 94 lililokuwa likitokea Banana kwenda Gongo la Mboto,.
“Watu 18 walijeruhiwa katika ajali hiyo na kupelekwa katika Hospitali ya Amana wakati wengine walipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Hali za majeruhi watatu zilikuwa mbaya,” alisema.
Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Neema Mwangomo alithibitisha hospitali hiyo ilipokea majeruhi tisa na mwili mmoja wa marehemu.
Mwiongomo aliwataja majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo kuwa ni Masiku Werema (45), Mohamed Juma (37), Adam Rashid (25) na Joshua Stephen (32).
Wengine ni Said Juma (17), Eliza Chacha (14), Maua Malick (48), Stella Mpahe (35) na Juma Mtally.
“Kati ya majeruhi hao, Adam Rashid alipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya hali yake kutengamaa,” alisema.
Mwangomo alisema majeruhi wengine bado wamelazwa wakiendelea kupatiwa matibabu.