Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:59 am

NEWS: AJALI YA TRENI YAUWA WAFANYAKAZI 5 WA SHIRIKA LA RELI NCHINI

Dar es Salaam. Wafanyakazi watano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) wamefariki dunia baada ya treni ya uokoaji kugongana na kiberenge.

Tarifa iliyotolewa leo na Shirika hilo imesema kuwa ajali hiyo iliyotokea jana Jumapili Machi 22, 2020 maeneo kati ya stesheni za Mwakinyumbi na Gendagenda iliua watumishi wanne papohapo na kujeruhi wawili.

“Watumishi wa TRC walikuwa sita, watumishi wanne wamefariki pale pale katika eneo la ajali na majeruhi wawili walifikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya (Magunga) Korogwe kwa huduma za kitabibu,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Majeruhi mmoja alifariki dunia akiwa hospitalini akipatiwa matibabu na kufikisha vifo vitano.


Taarifa hiyo imewataja waliofariki dunia kuwa ni; Ramadhani Gumbo, Fabiola Moshi, Joseph Komba, Philip Kajuna na George Urio.
Kuhusu maandalizi ya mazishi ya watumishi hao shirika limesema litatoa taarifa likisema uchunguzi utafanywa kubaini chanzo cha ajali hiyo.