- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AJALI YA NDGE YA TEHRAN YAUWA WATU 170 KUTOKA MATAIFA MATATU
Takribani watu 170 wamefariki dunia katika ajali ya ndege aina ya Boeing 373 ya shirika la ndege la Ukraine International Airlines. Ndege hiyo imeanguka nchini Iran leo Jumatano muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa waTehran ikielekea Kiev, vyombo vya habari vya Iran vimeripoti.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kuwa hakuna aliyenusurika katika ajali hiyo.
"Abiria wote na wafanyakazi" wa Boeing 737 ya shirika la ndege la Ukraine International Airlines "wamefariki dunia," Bw Zelensky ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Muda mfupi kabla, afisa mwandamizi kwenye wizara ya Mambo ya Nje ya Ukrainewa, Vassyl Kyrylytch, amelithibitisha shirika la habari la AFP kwamba hakuna aliyenusurika katika jalai hiyo.
Amesema kuwa "kulingana na takwimu za awali, kulikuwa na watu 168 katika" ndege hiyo ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Iran kwenda Kiev.
"Hakuna matumaini yoyote ya kuwapata watu walionusurika katika ajali ya ndege hiyo PS-752 iliyokuwa ikisafiri kutoka Tehran kwenda Kiev," mkuu wa shirika la mwezi mwekundu, ISNA, Morteza Salimi amesema.
Ajali hiyo ilisababishwa na "matatizo ya kiufundi," Press TV imemnukuu Ali Khashani, msemaji wa mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeiny, nchini Iran