- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AHADI ZA RAIS MAGUFULI WAKATI AKIOMBA KURA YA URAIS ZAWATESA WABUNGE
Dodoma: AHADI zilizotolea na Rais Dk.John Magufuli wakati wa kipindi cha kampeini cha kuomba kura ya kuwa rais zimeanza kuwatesa wabunge kutokana na ahadi hizo kutotekelezwa kwa wakati.
Hali hiyo imejitokeza leo bungeni baada ya Mbunge wa Bukombe Dotto Biteko (CCM) kuhoji ni lini ujenzi wa barabara za halimashauri ya Bukombe mji wa Ushirombo utaanza kama ilivyo tolea ahadi na rais Dk. Magufuli wakati akiomba kura.
Biteko alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza huku akitaka serikali iweke wazi ni lini ahadi ya rais itatekelezwa ya ujenzi wa barabara zilizopo katika mji wa Ushirombo katika halmashauri ya Bukombe.
Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni lini ahadi za rais zitatekelezwa kwani kwa sasa imebaki miaka mitatu tu na utekelezaji wa ujenzi wa barabara haujaanza kutekelezwa katika mji wa Ushirombo katika halmashauri na Bukombe.
“Wakati wa Kampeini za mwaka 2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alihaidi kilometa 5 kwenye mji wa Ushirombo,Je ni lini ahadi hiyo itatekelezwa” alihoji.
Akijibu maswali la nyongeza la mbunge huyo Naibu wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,Edwini Mgomyani amesema ahadi zote za Rais zitatekelezwa ndani ya miaka mitano.
Aidha amesema pamoja na mambo mengine wakati upembubuzi yakinifu ukiendelea wakandarasi wanatakiwa kuwa katika maeneo ya kazi ili kuharakisha utendaji wa kazi kuwa sahihi.
Serikali imekusanya ahadi zote za viongozi na kuweka utaratibu wa jinsi ya kuzitekeleza ikiwemo ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara zenye jumla ya urefuwa kilometa tano zilizoahidiwa na rais Magufuli mwaka 2015 mjini Ushirombo.