- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AFISA WA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR ABURUZWA KORTINI
Zanzibar. Ofisa wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Abdallah Juma Abdallah (46) amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa Vuga akikabiliwa na shtaka la kubaka mwanafunzi wa kidato cha nne na kumdunga mimba mwanafunzi huyo.
Kesi hiyo namba 123/2019 imesomwa juzi April 9 mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Fatma Muhsin Hakimu.
Hakimu Fatma alisema kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana mshtakiwa atapelekwa rumande kwa wiki mbili kesi yake itakapoanza kusikilizwa.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi, Thobias Sedeyoka amesema baada ya kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo walikabidhi jalada kwa mwendesha mashtaka wa Serikali. Sedoyeka ameyasema hayo leo Alhamisi Aprill 11,2019 akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Mshtakiwa huyo anadaiwa kumbaka msichana mwenye miaka 16 aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha nne na kumpa mimba.