Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:41 am

NEWS: AFISA WA TAKUKURU ABURUZWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA YA SH. 200M

Afisa wa ngazi ya Juu kutoka katika Taasisi yanye dhamana ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru), Cosmas Batanyita (44), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka saba miongoni likiwemo la kuomba rushwa ya Shiling Milioni 200 na kutakatisha fedha.

Afisa huyo ni mkazi wa Chamazi, jijini Dar es Salaam amefikishwa mahakamani hapo, leo Ijumaa Agosti 9, 2019 na kusomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina.

Image result for TAKUKURU dar es salaam

Wakili mkuu wa Serikali, Paul Kadushi akisaidiana kusomewa mashtaka yake na Wankyo Simon amedai mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 76/2019.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili mshtakiwa huyo ni kushawishi, kuomba rushwa na kutakatisha fedha, ambapo anadaiwa kuyatenda kati ya Februari 9, 12 na 24, 2019.

Katika shtaka la kuomba rushwa, Batanyita anadaiwa Februari 9, 2019 eneo la Upanga, Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa Takukuru alishawishi na kuomba rushwa ya Sh200 milioni kutoka kwa Hussein Gulamal Hasham ili aweze kuharibu ushahidi katika kesi ya ukwepaji wa kodi ilivyokuwa inamkabili Hasham. Image result for mahakama ya kisutu

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili, hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana. Upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo wa naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 23, 2019 itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande.