- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AFISA TAKUKURU FAKE MBARONI MJINI DODOMA
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Dodoma inamshikilia Simon Mapunda mkazi wa Dodoma kwa tuhuma za kujifanya afisa wa taasisi hiyo Mkoa wa Dodoma, kinyume cha kifungu namba 36 cha sheria ya kuzuia ya kuzuia na kupambambana na rushwa.
Taarifa hiyo imetolewa leo Mei 7, 2020 na Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma
Kibwengo amesema kuwa Mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kuwalaghai watu mbalimbali na kuwadai fedha na kusisitiza kuwa atawasaidia kupata ajira ndani ya Takukuru na ofisi zingine za serekali.
Kibwengo alifafanua kuwa Takukuru iliweka mtego mara baada ya kaka wa mtoa taairfa kuahidiwa ajira ya udereva ndani ya takukuru Dodoma. Baada ya kuahidiewa ajira ya udereva kaka wa mtoa taarifa alikuwa hana leseni ya udereva class c ndipo mtuhumiwa akamwambia atoe laki tatu (300,000) ili amsaidie pia kupata leseni hiyo