- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AFISA POLISI MBARONI KWA UTAKATISHAJI WA PESA
Dar es Salaam. Ofisa wa Polisi nchini Tanzania, Emmanuel Mkilia(44) na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kutakatisha fedha kiasi cha Sh798 milioni mali ya Jeshi la Polisi Tanzania.
Mbali na Mkilia, washtakiwa wengine ni mtaalamu wa Tehama, Donald Mhaika (39) mkazi wa Kinondoni, Abdi Ally (48), mkazi wa Ilala na Mohyadin Hussein (56) mfanyabiashara na mkazi Mikocheni.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao, leo Januari 6, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani hiyo, Salum Ally.
Hata hivyo, kabla ya kusomewa mashtaka hao, hakimu Ally, alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama ya Kisutu kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa DPP.
Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisaidiana na Janeth Magoho, alidai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kesi ta uhujumu uchumi namba 2/2020.