- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: AFISA BANDARI KORTINI KWA WIZI WA BILIONI 5
Dar es salaam: Aliyekuwa mtumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Stephen Mtui, ameburuzwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam akikabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya zaidi ya Sh bilioni 5.
Mshtakiwa huyo aliyefikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Vicky Mwaikambo.
Akimsomea mashtaka, yake na Wakili wa Serikali, Faraja Nguka alidai mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka matano; mawili ya kughushi, wizi, kuisababishia mamlaka hasara na utakatishaji wa fedha.
Mtui anadaiwa kati ya Julai 6, 2014 na Julai 8, 2014 katika eneo la bandari kavu ya AMI, Dar es Salaam, mshtakiwa alighushi nyaraka akionyesha kuwa Kampuni ya Anchor Clearing and Forwarding imelipa TPA Sh milioni 2.6 kupitia Benki ya CRDB kama tozo ya bandari huku akijua si kweli.
Katika shtaka la pili, anadaiwa kuwasilisha nyaraka hiyo ya kughushi na shtaka la tatu anadaiwa kati ya Julai 2014 na Aprili 2015 akiwa mtumishi wa TPA, aliiba zaidi ya Sh bilioni 5 mali ya mamlaka hiyo.
Shtaka la nne mshtakiwa huyo anadaiwa kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya zaidi ya Sh bilioni 5 akiwa aneo la bandari kavu ya AMI.
“Mheshimiwa hakimu, shtaka la mwisho la utakatishaji fedha haramu, mshtakiwa akiwa na wenzake kati ya Julai, 2014 na Aprili 2015 katika eneo la Bandari ya AMI, wanadaiwa kufanya miamala ya zaidi ya Sh bilioni 5 wakijua fedha hizo ni zao la wizi,” alidai Wakili Nguka.
Baada ya kumaliza kusoma mashtaka, alidai upelelezi haujakamilika hivyo aliomba kesi ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Mwaikambo alisema kutokana na shtaka linalomkabilili mshtakiwa, mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi hapo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) atakapotoa kibali cha kusikiliza.
Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Januari 20 kwa kutajwa na mshtakiwa kapelekwa rumande.