- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ADO SHAIBU ACHAGULIWA KUWA KATIBU MKUU ACT WAZALENDO
Dar es salaam: Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho mara baada ya kupata kura za ndio 75, sawa na 100%. Hii ni baada ya Mpinzani wake Ndugu Joram Bashange kwa ridhaa yake kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.
Ado amechaguliwa Leo na katika Kikao cha Halimashauri kuu ya chama cha ACT Wazalendo kilichoketi leo Machi 16, 2020 katika ukumbi wa mikutano wa mlimani City jijini Dar es salaam.
Baada ya kutangazwa mshindi katika Kinyang'anyiro hicho ADO aliwashukuru sana wajumbe wote kwa kumpa dhamana hiyo na kuahidi kufanya kazi kwa kwenda kwa wananchi (field) zaidi kuliko kukaa ofisini.
"Nawashukuru wajumbe wa Halmashauri wa Chama chetu kwa kunichagua kuwa Katibu Mkuu wa chama chetu. Ushindi huu wa %100 ni ishara ya imani yenu kubwa kwangu, "Ukatibu wangu utakuwa ni ukatibu wa Field." amesema Ado
"Hiki ndio chama pekee kilichoonesha kwa vitendo nia ya dhati ya kuwapa nafasi vijana. Hivyo vijana wote njooni kwenye chama chetu. Hiki chama chenu, Watanzania wanaitazama ACT Wazalendo kama chama mbadala."