- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ACT YAWATAKA POLISI KUMTUMIA ZITTOKABWE WITO WA MAADISHI
Dar es Salaam: Chama cha Upinzani nchini Tanzania ACT Wazalendo kimesema ili Zitto aripoti polisi ni lazima atumiwe wito maalum wa kimaandishi unaotambulika kisheria na si kupitia vyombo vya habari kama alivyotumia RPC kinondoni Mussa Taibu.
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema, “Zitto hajapokea wito maalum wa kuitwa, RPC ametoa wito wa kisiasa. Na wakifanya hivyo Zitto atakwenda kuitikia wito huo lakini kama ni hivi (kupitia vyombo vya habari) hawezi kwenda.”
Kauli hiyo ya ACT imekuja mara baada ya Jana Ijumaa Agosti 17, 2019 kamanda wa polisi wilayani ya Kinondoni, Mussa Taibu kuliambia gazeti la Mwananchi kuwa Zitto anatakiwa kufika kituoni kwa mahojiano.
Kamanda Taibu alitoa kauli hiyo baada ya polisi kuzuia mkutano wa mbunge huyo wa Kigoma Mjini na waandishi wa habari ulikuwa ufanyike katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, Zitto alipanga kuzungumzia mkutano wa 39 wa wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) unaoendelea nchini.