- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ACT WAZALENDO YAWEKA REKODI, YAANZISHA MATAWI 675 NDANI YA SIKU 5
Kiongozi Mkuu wa chama cha ACTwazalendo Zittokabwe amesema ndani ya siku 5 wamefanikiwa kuanzisha Jumla ya matawi mapya 675 ambapo Wanachama wapya wa chama hicho wanaohitaji kadi mpaka sasa ni 125,000 hii ni kwa upande wa Zanzibar pekee, kati ya wanachama hao wanachama 20,000 wameshapokea kadi mpaka kufikia sasa.
Leo Jumamosi Kiongozi huyo alikuwa kwenye Ziara ya wilaya 11 katika jimbo la Chambani Mkoa wa Kusini Pemba Kukitambulisha chama akiambatana na aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
Katika Hotuba yake Zitto amesema kuwa Pemba ilikuwa ngome ya CUF chini ya uongozi wa Maalim Seif. Kwa hivyo, kitendo cha mliokuwa wanachama wa CUF nyote kwa umoja wenu kujiunga na jukwaa jipya la siasa la ACT Wazalendo kinaifanya Pemba sasa kuwa ngome ya ACT." Hili ni jambo kubwa sana kwa chama chetu"
"Tumewapokea kwa moyo mkunjufu na mjihisi mmefika na mko nyumbani ndani ya ACT. Karibuni sana!"
"Kisiwa cha Pemba na wananchi wa Pemba mna historia kubwa sana katika mapambano ya kupigania haki, demokrasia na utu. Pemba imekuwa ALAMA ya mapambano ya kupigania haki na demokrasia kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi'' amesema Zitto